0
Msanii wa muziki, Matonya amedai bado kuna baadhi ya wadau wa muziki wanawabania wasanii wenye vipaji.
matonya
Akiongea na Bongo5 wiki hii, Matonya amedai yeye ameshazoea hali hiyo ndio maana anapambana kwa kila hali ili kufanya vizuri kwenye game.
“Hii hali inaathiri na tumeizoea, dunia ndo inaenda hivyo.” Alisema Matonya. “Kwenye dunia kuna vitu vinatokea vya halali na vingine sio vya halali kwa hiyo hata kama una nguvu huwezi kuwapinga wenye nguvu zaidi yako ila tunapambana ili kupata kile ambacho tunastahili kupata,”
Aliongeza, “Wanyonyaji wapo kila sehemu, kwa wachezaji wa mpira wapo, maofini wapo, yaani kila sehemu ila chamsingi tu nikufanya kazi na sera yetu kwa pamoja ni kuitangaza nchi kimataifa. Kwa hiyo sisi kama wasanii tufanye kazi kwa bidii na washikadau wawe washikadau sio washika nyau.,”
Kwa sasa muimbaji huyo anamiliki kundi la wasanii liitwalo ‘Black Image’ ambalo hivi karibuni limeachia wimbo ‘Sugua Benchi’.

Post a Comment

 
Top