Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33, alifunga bao la kuongoza katika mchezo wa ligi uliochezwa jana dhidi ya Akhisar ambao walikubali kufungwa mabao matatu kwa moja.
Katika dakika ya 37 Van Parsie alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kupata jeraha la jicho na kulazimika kutolewa nje ya uwanja kwa usaidizi wa watu wa huduma ya kwanza, baada ya kugongana na mchezji wa timu pinzani.
Baada ya mchezo kumalizika uongozi wa Fenerbahce ulitoa taarifa njema kwa mashabiki ambazo zilieleza Van Parsie anaendelea vizuri.
“Alipatwa na tatizo la jicho lakini kwa uchunguzi wa awali imeonekana sio kubwa sana,” ilieleza taarifa ilitotolewa na daktari Burak Kunduracıogl.
“Tumejiridhisha jeraha lake halitomuweka nje kwa muda mrefu, lakini kwa siku kadhaa atakua katika uangalizi wa kimatibabu.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.