0
Mastaa kadhaa wa Tanzania walitumia time yao kumuongelea rapper Chidi Benz akiwemo staa wa bongo hiphop Fid Q ambaye alisema Chidi Benz asisimangwe wala kunyooshewa kidole kwa kutelezea kwenye utumiaji wa dawa za kulevya bali asaidiwe… ambapo baada ya kuonekana kwenye D’Wikend chat show ya CloudsTV watu walianza kusambaza picha zake za zamani na muonekano wake wa sasa akionekana amepungua mwili kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya.

Meneja Babu Tale ambaye anawasimamia Wasanii wa TipTop Connection pamoja na Diamond Platnumz amepigiwa makofi ya pongezi na watu wengi akiwemo mkuu wa mkoa wa Dar es salaam baada ya kuamua kumpeleka Chidi Benz kwenye nyumba ya matibabu (REHAB) huko Bagamoyo ikiwa ni siku chache tu baada ya Tale kuumizwa kuona Chidi Benz yuko kwenye hali hii kupitia hii show ya CloudsTV.


.inaendelea

MTAZAME BABU TALE ALIVYOMPELEKA CHIDI BENZ KWENYE NYUMBA YA MATIBABU (REHAB) BAGAMOYO…na ayotv

Post a Comment

 
Top