Habari na Imelda mtema
Unapowazungumzia wanamitindo wakubwa Bongo, huwezi kuacha kumtaja Martin Kadinda. Licha ya kupata umaarufu kupitia kazi yake, Kadinda aling’ara zaidi alipoanza kumsimamia supastaa mkubwa Bongo, Wema Sepetu akiwa meneja wake.
Kazi yake ya uanamitindo imempatia tuzo kibao zikiwemo Mwanamitindo Bora Afrika Mashariki 2015, Mbunifu Bora wa Mavazi ya Kiume Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo na nyingine nyingi.
Juzikati alipiga stori na gazeti hili na kufunguka mambo kibao kuhusu maisha yake na kueleza sababu inayomfanya asipende kuonekana na mademu. Shuka nayo:
Amani: Mambo vipi Kadinda! Unaweza kumwambia msomaji umaarufu wako umetokana na nini?
Amani: Umaarufu wako ulitokana na nini?
Kadinda: Ulitokana na na kazi yangu ya ubunifu wa mavazi ndio chanzo cha umaarufu wangu.
Amani: Kuna ukweli wowote kuwa jina lako lisingekuwa kubwa kama usingekuwa meneja wa Wema?
Kadinda: Ukubwa wa jina langu umetokana na kazi zangu ila kwa kiasi kikubwa ni kwa watu maarufu niliowavalisha wamenisaidai sana mimi kufahamika na pia moja malengo yangu ya kummeneji wema ni kuongeza wigo katika biashara zangu na kiukweli amenisaidia sana ninamshukuru siku zote kwa hilo kila wakati.
Amani: Changamoto gani unakutana nazo kama meneja wa staa mkubwa Bongo?
Kadinda: Unapokuwa una hela unaishia kufanya kazi kutokana na kile anachotaka mhusika pia ni ngumu sana kumsimamia mtu ambaye ana malezi tofauti na uliyolelewa wewe hivyo inakuchukua muda sana kuelewana na kuendana njia moja na pia binadamu tunaishi kutokana na kile tunachokiamini hivyo changamoto za watu wanaotuzunguka na utofauti wa ndoto ndio changamoto zenyewe.
Amani: Kipindi cha Wema yupo na aliyekuwa kigogo wa Ikula Ck, vilizuka vitu vingi sana kuwa uliweza kujenga nyumba kwa kutumia hela zake wakati yeye hana nyumba unazungumziaje hilo?
Kadinda: Naomba nirekebishe kauli za watu mimi sina nyumba nina kibanda ambacho nimejenga kwa nyuma ya nyumba yetu familia hivyo huwa napaita banda la uani na hata hivyo nimejenga kipindi cha ‘ Single Buttons’ na n ilikuwa sijaanza kufanya kazi na Wema kama meneja wake.
Amani: Sasa kama wewe meneja wake kwanini kwa kipindi chote hujaweza kusimamia kuwa na nyumba yake mwenyewe?
Kadinda: Unajua suala la nyumba kwa Wema kutokuwa nayo mpaka sasa ni aina ya nyumba anayotaka kujenga inahitaji hela nyingi sana lakini kwa vile tayari ana miliki kiwanja hivi karibuni watu wataiona hiyo nyumba ninayoongelea.
Amani: Ni mafanikio gani umeyapata mpaka sasa hivi kupitia unamitindo?
Kadinda: Kwa kweli sijafika sehemu ambayo naweza kusema nina mafanikio ila kikubwa nimeweza kuitangaza nchi yangu kupitia sanaa yangu hiyo na pia kuwa na mahusiano mazuri na wabunifu wakubwa toka nchi mbalimbali duniani na nimeweza kutembea sehemu tofauti.
Amani: Unazungumziaje watu kusema kuwa husimamii kazi za Wema ipasavyo kwa maana anafanya vitu vingine ambavyo sivyo?
Kadinda: Wema sio mtoto mdogo mimi napaswa kumshauri tu na kumuonesha njia suala la yeye kutofuata ninachomueleza ni maamuzi yake binafsi na pia ikumbukwe pia nafasi ya kummeneji Wema sio kwamba natembea nayo kama kuna mtu anahisi anaweza kufanya hivyo anakaribishwa.
Amani: Vipi kuhusu harusi yako maana ilivuma baadae ikapotea na vipi kuhusu mchumba wako huyo?
Kadinda: ( kicheko) Hilo watu walizusha tu ,muda w akuoa mimi ukifiuka tu wataona picha tu kwetu suala la ndoa ni la kifamilia tu zaidi hao wengine wataishia tu kulike picha kwenye mitandao ya kijamii.
Amani: Kuna video ilivuma hivi karibuni ikimuonyesha Wema na mwanamitindo Calisah wakiwa kwenye picha tata unalizungumziaje hilo kama meneja?
Kadinda: Mimi sijaiona nimesikia tu na hata kama ningekuwa nimeona nadhani Wema, Wema peke yake ndio anapaswa kutoa majibu ya kuhusu video hiyo maana ni maisha yake halisi.
Amani: Baada ya kutoa nguo yako aina ya Kwachukwachu unejipanga na kitu gani kingine?
Kadinda: Inachukua miaka miwili kuja na vazi jipya kwahiyo tukutane 2017.
Amani: Nakumbuka kama kipindi cha nyuma ulishawahi kuwa meneja wa Lulu ni sahihi?
Kadinda: Hapana Lulu ni mtu wangu wa karibu tangu tupo shule ni kama mdogo wangu na tunashauriana vitu mbalimbali.
Amani : Hivi karibuni ilidaiwa mlikuwa kwenye mgogoro mzito na Wema mpaka hamkuwa mnazungumza vipi kuhusu hilo,na pia hujafikiria kuwakalisha pamoja Muna na Wema wakamaliz atofauti zao?
Kadinda: Migogoro yangu na Wema inatokea mara nyingi tu kwa hiyo ni kawaida kwetu kuhusu Muna na Wema sio mimi niliwakutanisha mwanzo kwenye urafiki wao hivyo watapatana wenyewe tu kwasababu migogoro kwa marafiki ipo tu.
Amani: Kama meneja Wema alishakuwa na marafiki kama Kajala, Wema, Snura na Aunt ungependa kati ya hawa ni yupi angekuwa lakini wa kudumu kwake.
Kadinda: Mimi ningemshauri dada zake au mama yake lakini pia unajua urafiki ni swala la mtu binafsi siwezi kusema yupi anamfaa, pia ili Wema aweze kufanikiwa zaidi anapaswa kufanya kazi zake mwenyewe.
Amani: Wanawake wengi wanakusema kuwa unaringa kwasababu hata ukiwaona wazuri huwatongozi japokuwa hujawahi kuonekana na mwanamke?
Kadinda: Naheshimu mwanamke hasa kwa kuwa naamini sio kila mwanamke nitakayekuwa nae kwa mahusiano ndo nitakayemuoa na hiyo kwasababu nina binti yangu mdogo sitaki akue akiona habari zangu za mahusiano sio malezi ninayomlea ndio maana familia yangu na mahusiano yangu nayaweka mbali na media.
Amani: Kama meneja ungetamani Wema awe na nafasi gani katika jamii?
Kadinda: Kila anayempenda Wema,anataka kuona akiwa na nyota inayong’aa Tanzania na Afrika nzima kwa ujumla hilo ndio ombi langu kwake tu.
Amani: Kuna ugomvi ulitokea kati ya wewe na mama Wema kwa madai kuwa ulipewa hela ya kumnunulia Wema kiwanja ukanunua kisichokuwa na hadi ya pesa uliyopewa vipi hilo?
Kadinda: Sijawahi kuigombana na mama Wema hayo ni maneno tu nagombanaje na mama sasa? Siwezi ni maneno tu.
Amani: Kumbe una mtoto nilikuwa sijui
Kadinda: ndio nina binti wa miaka nane sasa nilimpata nikiwa shule.
Amani: Nakushukuru sana Kadida kwa ushirikiano wako?
Kadinda: Asante sana.
Post a Comment