Ngiri ama hernia ni tatizo linalo wakabili wanaume wengi duniani. Moja kati ya dalili kuu za tatizo la ngiri ni pamoja na kusinyaa kwa korodani moja au zote, kusinyaa kwa maumbile ya kiume.
Kama ilivyo kwa magonjwa mengine mengi, tatizo la ngiri linaweza kutibika kwa kutumia dawa mbalimbali za asili.
Ganda la tunda la upupu. Ndani yake zinakaa mbegu saba.
Ipo miti mingi sana inayo weza kutumika kama tiba ya tatizo la ngiri. Katika makala haya, nitaelezea kuhusu miti kumi ambayo imefanyiwa utafiti wa kisayansi na kuthibitika kuwa na uwezo wa kutibu na kuponyesha kabisa tatizo la ngiri. Kati ya miti hiyo, umo pia mti wa upupu ambao unajulikana sana kwa sifa yake ya kuwasha sana.
Miti hiyo ni kama ifuatavyo :
1. MULIWANIFWENGI :
Mti wa Muliwanifwengi hapa ukiwa umetoa matunda. Matunda ya mti huu pia ni dawa ambayo husaidia kusafisha damu.
Hili ni jina la lugha ya kinyamwezi. Wanyamwezi ni wenyeji wa mkoa wa Tabora, ambao unapatikana magharibi wa nchi ya Tanzania. Mti huu una uwezo mkubwa sana wa kutibu na kuponyesha kabisa tatizo la ngiri.
Muliwanifwengi
Jinsi unavyo tumika; mgonjwa anachukua mizizi anachemsha pamoja na maji kisha anatumia kunywa mara tatu kwa siku asubuhi mchana na jioni kwa muda wa siku thelathini.
Mbali na kutibu tatizo la ngiri, mti huu pia una uwezo wa kutibu ugonjwa wa kaswende pamoja na kusafisha mishipa ya damu.
Chipukizi la Muliwanifwengi ambalo bado halijakomaa
2.MUSISIGULU : Kama ilivyo kwa mti wa Muliwanifwengi, jina la mti wa Msisigulu linatokana na lugha inayo tumiwa na watu kutoka kabila la wanyamwezi wa mkoani Tabora.
Mti huu umefanyiwa utafiti wa kisayansi na kuthibitika kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu na kuponyesha kabisa tatizo la ngiri.
Pamoja na ngiri, mti wa Musisigulu, hutibu pia matatizo ya mapafu.
Jinsi ya kutumia mti wa Msisigulu katika tiba ya ngiri, chemsha mizizi yake kwenye kisha tumia kunywa mara tatu kwa siku kwa siku thelathini.
Upupu
3. MUMULIMULI : Mumulimuli ni jina la kinyamwezi. Mti huu umethibitishwa kisayansi kuwa na uwezo wa kutibu tatizo la ngiri, minyoo ya tumboni, kaswende pamoja na kisonono.
Jinsi ya kutumia mti huu, chemsha mizizi yake kisha tumia kunywa mara mbili kwa siku asubuhi na jioni kwa siku thelathini.
4.Muzegezega : Mti huu pia umefanyiwa utafiti wa kina na kuthibitika kuwa na uwezo mkubwa wa kutibu na kuponyesha kabisa tatizo la ngiri.
Pamoja na kutibu ngiri, mti wa Muzegezega, una uwezo wa kutibu pia magonjwa mengineyo kama vile ; Kufeli kwa moyo, Homa Ya Manjano, Kikohozi, Pumu, Mkamba ( Bronchitis ), Matatizo katika ubongo pamoja na Degedege.
5. Kasolanhanga au Sawi au Asparagus ; Huu ni mmea uliothibitika kisayansi kuwa na uwezo mkubwa sana wa kutibu na kuponyesha kabisa tatizo la ngiri. Katika lugha ya kinyamwezi, hujulikana kama Kasolanhanga au Sawi , lakini katika kiingereza, hujulikana kama Asparagus.
Mmea huu ambao ni jamii ya mbogamboga, mbali na kutibu tatizo la ngiri, hutumika pia kama tiba ya ugonjwa wa Gono.
Jinsi inavyo tumika, mgonjwa atachemsha mizizi ya mti huu kwenye maji, kisha atatumia kunywa asubuhi mchana na jioni kwa muda wa siku thelathini.
6. Nyanya Chungu : Nyanya chungu ni mti wenye faida nyingi sana katika afya ya mwanadamu. Karibu kila kiungo kinacho patikana katika mmea wa Nyanya Chungu ama Ngogwe hutumika kama tiba kwa mwanadamu. Kuanzia matunda, majani, hadi mizizi.
Kujitibu tatizo la ngiri kwa kutumia mmea wa Nyanya Chungu, chukua mizizi yake kisha ichemshe kwenye maji , halafu tumia kunywa maji hayo, mara tatu kwa siku, asubuhi na jioni kwa siku thelathini. Tatizo lako litapona kabisa.
7. Bumu ama Upupu ; Bumu ni lugha inayo tumiwa na waluguru wenyeji wa mkoa wa Morogoro, wakimaanisha mti wa Upupu. Mti wa upupu unajulikana zaidi kwa sifa yake moja kubwa, ambayo ni kuwasha sana.
Pamoja na kuwa na sifa ya kuwasha, mti wa upupu una faida nyingi sana za kitabibu pamoja na kiuchumi. Katika makala haya ya leo, nitaelezea jinsi mti wa upupu unavyo tumika kama tiba ya tatizo la ngiri.
Kutibu tatizo la ngiri kwa kutumia mti wa upupu, chukua mizizi au majani ya mti wa upupu ulio komaa, kisha chemsha halafu tumia kunywa mara mbili kwa siku asubuhi na jioni kwa siku kumi na nne., na tatizo lako litapona. Waluguru kutoka mkoani Morogoro, wanatumia sana mti wa upupu kama tiba ya ngiri. ( TAHADHARI : WATU WENGI WANASHINDWA KUTUMIA VIZURI MTI VIZURI KAMA TIBA. HIVYO HAUSHAURIWI KUUTUMIA MWENYEWE BILA KUPATA USHAURI NA MSAADA WA MTAALAMU, NA BADALA ZINGATIA MATUMIZI YA MITI MINGINE )
Mbali na kutibu ngiri, mti wa upupu una uwezo pia wa kutibu maradhi ya “Parkinson Desease”
8. Kiberuberu : Huu ni mti mwingine ulio fanyiwa utafiti na kuthibitishwa kitaalamu, kuwa na uwezo wa kutibu na kuponyesha kabisa tatizo la ngiri. Kiberuberu ni jina la mti huu katika lugha ya kiluguru. Katika lugha hiyo hiyo ya kiluguru, mti huu hujulikana kama Mguhu.
Mti huu hutumika kwa mgonjwa kuchemsha mizizi yake na kisha kutumia kwa kunywa, mara tatu kwa siku kwa siku thelathini.
9. Luhalamila au Luhambamti : Hili ni jina kutoka katika lugha ya Kiluguru inayo zungumzwa na watu kutoka jamii ya waluguru wanao patikana mkoa wa Morogoro, nchini Tanzania. Mti huu umefanyiwa utafiti wa kisayansi na kuthibitika kuwa na uwezo wa kutibu na kuponyesha kabisa tatizo la ukosefu na nupungufu wa nguvu za kiume
Jinsi ya kutumia tiba hii, mgonjwa anatakiwa kuchemsha majani yake yakiwa mabichi na kisha kutumia kunywa mara tatu kwa siku, asubuhi, mchana na jioni kwa siku thelathini.
10.Luziwana : Waluguru wa mkoani Morogoro, wanautumia sana mti huu kama tiba ya tatizo la ngiri. Mbali na kutibu ngiri, mti wa Luziwana hutibu magonjwa mengineyo kama vile kuharisha pamoja na maumivu ya tumbo.
Mgonjwa anashauriwa kuchemsha mizizi ya mti huu na kisha kutumuia kunywa mara tatu kwa siku kwa siku thelathini.
KAMA NILIVYO DOKEZA, HAPO AWALI, TANZANIA TUMEBARIKIWA KUWA NA MAELFU YA MITI YENYE UWEZO WA KUTIBU MAGONJWA NA MATATIZO MBALIMBALI YA KIAFYA YANAYO MKABILI MWANADAMU. KATIKA TATIZO LA NGIRI PEKEE, KUNA MAMIA KWA MAMIA YA MITI INAYO TUMIKA KUTIBU TATIZO HILO. KATIKA MAKALA HAYA NIMEELEZEA MITI KUMI TU. KATIKA MAKALA ZA USONI, NITAELEZEA PIA MITI MINGINE, AMBAYO INATIBU TATIZO LA NGIRI.
MAKALA HAYA YAMELETWA KWENU KWA HISANI YA DUKA LA NEEMA HERBALIST. DUKA LINALO UZA DAWA MBALIMBALI ZA ASILI. TUNAPATIKANA UBUNGO JIJINI DAR ES SALAAM, JIRANI NA SHULE YA MSINGI UBUNGO NATIONAL HOUSING, NYUMA YA JENGO LA UBUNGO PLAZA.
Post a Comment