0
Shirikisho la Kandanda Duniani, FIFA limemfungia maisha kutojiusisha na masuala yote ya soka Katibu mkuu mtendaji wa zamani wa Concacaf Chuck Blazer. Chuck Blazer, 70 alikuwa akifanya udukuzi kwa niaba ya FBI katika Shirikisho la Soka Dunia kwa kipindi cha miaka miwili. Alikubali kuwafanyia kazi viongozi wa Marekani baada ya kugunduliwa na mamlaka ya kodi kwa kushindwa kulipa kodi kwa mamilioni ya fedha aliyopitisha mlango wa uani kwa kipindi cha miaka ishirini na moja akiwa kama Katibu mkuu mtendaji wa Concacaf, ambalo ni Shirikisho la Soka la Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kati na Caribbean.
Mpaka sasa, maofisa tisa wa FIFA waliochaguliwa pamoja na wadau watano wa uongozi wa soka wameshtakiwa rasmi kwa tuhuma za kashfa ya rushwa, hasa kuhusiana na utoaji wa Kombe za Dunia, haki za masoko na televisheni.

Post a Comment

 
Top