0
Jeshi la Polisi nchini limesitisha maandamano ya aina yoyote wakati wote wa zoezi la kuchukuwa fomu, kutafuta wadhamini mikoani na hata wakati wa kurejesha fomu ili kuweka hali ambayo haitaleta usumbufu au kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.

Akitoa taarifa hiyo jana  mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam naibu inspekta jenerali wa polisi Abdulrahman Kaniki alisema  uamuzi huo umefikiwa baada ya jeshi hilo kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya usumbufu uliojitokeza wa watu kushindwa kuingia maofisini na wengine kushindwa kufika kwa wakati katika shughuli za kiuchumi na kijamii kutokana na misafara mirefu iliyosababishwa na vyama vya Chadema na CCM wakati wagombea wao walipokwenda kuchukuwa fomu.

Aidha amesema jeshi hilo halina ugomvi na chama chochote cha siasa wala mchakato wa uchaguzi unaoendelea isipokuwa lengo lao ni kutengeneza mazingira mazuri ili vyama vyote viweze kutekeleza majukumu yao vizuri na kwa kufuata sheria za nchi.

Akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari likiwemo la tuhuma zinazoenezwa kwenye mitandao ya kijamii na ambazo baadhi ya wanasiasa wanazizungumzia juu ya askari polisi kutakiwa kupeleka shahada zao za kupigia kura ili namba zao za uandikishwaji zichukuliwe naibu inspekta kaniki alisema  swala hilo halina ukweli wowote.

Post a Comment

 
Top