0
Msanii wa muziki wa Kundi la TMK Wanaume Family, Chege Chigunda anajipanga kuachia wimbo mpya ambao atafunga nao mwaka 2016.
chege
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Waache Waoane’ aliomshirikisha Diamond, amesema muziki umebadilika hivyo msanii hatakiwi kukaa muda mrefu bila kuachia wimbo.
“Kwangu mimi nasema bado mwaka haujaisha kwa sababu muziki umebadilika sana, msanii anatakiwa asikae muda mrefu bila kuachia wimbo, binafsi sina muda wakupumzika ni ngoma baada ya ngoma. Kwa hiyo kabla ya mwaka kuisha nitaachia wimbo mwingine mpya,” alisema Chege.
“Kwa hiyo mashabiki wangu wajue Chege bado nakuja tena waandae tu masikio yao kwa sasa nipo studio katika maandalizi ya mwisho ya wimbo mpya ambao utatoka baada tu ya kukamilika,”
Chege ni mmoja kati ya wasanii waliofanya vizuri katika tamasta la fiesta lililofanya weekend iliyopita katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam.

Post a Comment

 
Top