0
Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa Ufaransa na klabu ya West ham, Dimitri Payet amesani tena mkataba mpya wa miaka mitano na timu yake hiyo.

Payet mwenye umri wa 28 alijiunga na West ham ya Jijini London msimu uliopita akitokea timu Marseille kwa dau la zaidi ya pauni milioni 10.

Wiki hii klabu yake ilizikataa taarifa zilizosambaa kuwa mchezaji huyo anataka mkataba mpya, huku mkataba wake wa kwanza pia ukiwa ni miaka mitano.

Mchezaji huyu kutoka Ufaransa amefunga mara 6 katika michezo 22 aliyocheza na kuiweka West Ham katika nafasi ya sita ya msimamo wa ligi kuu ya England.

David Sullivan, mmiliki wa timu hiyo amesema “tutafanya chochote kuwabakiwa wachezaji wetu wazuri na Payet ni mchezaji mzuri.”

Post a Comment

 
Top