0

Katika kujiweka fiti au tuseme kujiweka sawa kwa ajili ya kuonekana mrembo ni kazi ambayo inahitaji muda na uvumilivu vinginevyo unaweza kuwa sawa na chizi yoyote aliyejiwekea si tu maleba bali na mwili usiotamanika. 

 Na kwa mwanamke ambaye ana mji wake, watoto , familia na kazi inayohitaji ukakamavu mkubwa huku akitakiwa kuonekana bomba namchangamfu ni dhahiri kuwa la ziada lazima lifanyike vinginevyo mahali fulani utapwaya.unaweza kupwaya ofisini, ukaonekana huna maana , unaweza kupwaya nyumbani mtoto mkubwa akashindwa kukuangalia mara mbili na unaweza kupwaya mtaani watu wakajiuliza hee mama fulani vipi mbona usafi unamshinda?ndio kusema katika hili unahitaji mwanamke kuwa makini sana. Inavyoonekana wanawake wengi wanapokuwa katika mtawanyiko wa mambo hujisahau kabisa na mara nyingi husahau kabisa kuwa wanahitaji kula nakufanya vitu fulani ili kujiweka fiti.Kimsingi wanawake wote wawe wanachapa kazi kama wazimu, wawe na familia, wawe na mtoto mkubwa wanatakiwa kujiweka safi na sawa muda wote pamoja na majukumu yao yaliyotawanyika. 
 1) suiku zote hakikisha una tunda wakati wa kifungua kinywa chako. Hiiinasaidia kuondoa sumu katika mwili wako na kusaidia kuondoa uchafuuliojiweka kwa namna inavyostahili. 
 2) Kunyw amaji ya kutosha , punguza chai na kahawa kufikia angalauvikombe viwiuli kwa siku na muda uliobaki kunywa vinywaji ambavyo nivya mizizi kama jasmine, chamoile tea. Vinywaji hivi katika mfumoi wajuisi ni dawa tosha kwa ngozi yako na ili ionekane ya ujana muda wotena isiwe kavu.
 3) Huku umri wako ukiwa unapanda,punguza vyakula vya nafaka na kulazaidi matunda na mbogamboga ili kupunguza uzito.
 4) hakikisha unatembea vya kutosha na kujinyoosha ili uwe na mwili wakuvutia, mwembamba na wenye nguvu za kutosha na wa ujana.
 5) Punguza uvutaji sigara na pombe kwani ni vitu viwili vinavyozeeshangozi kwa kasi.
 6) Ongeza vyakula vya samaki katika chakula chako au aina yake
 7) Uwe unakula na mizizi inayokabiliana na uzee kama tulsi, amla, ashwagandha 
 8) Jipatie vitamu vya asili kama asali na raisins. 
 9) Kula vyakula vyako unavyopenda vya hovyo angalau mara moja kwa wiki 
 10) Kujisikia vyema ni namna bora za kukufanya uwe mwanamke bomba naanayevutia muda wote. 
 NB:Kujisikia vyema huku ni kujipenda mwenyewe kama hujipendi huwezi kuvutia na kama unaridhika kwa sababu ya kuridhika una tatizo kwelikwel

Post a Comment

 
Top