Kiongozi wa kundi la wapiganaji Waislamu wa Nigeria, Boko Haram, amekanusha ripoti kwamba ameuwawa au kutolewa katika uongozi.
Katika rikodi ya sauti inayoaminiwa ni ya Abubakar Shekau, anaeleza kuwa ni uongo ripoti kwamba amefariki, amelemaa au ni mgonjwa.
Juma lilopita rais wa Chad, Idriss Deby, alisema kuwa Boko Haram imemteua kiongozi mpya na kuzusha tetesi kwamba Bwana Shekau ameuawa.
Ujumbe wake huo umewekwa katika mitandao ya kijamii na ulilengwa kwa kiongozi wa Islamic State, Abu Bakr al-Baghdadi.
Awali mwaka huu, Boko Haram ilitangaza kuwa ni tiifu kwa IS.
Post a Comment