MREMBO kutoka nchini Kenya, Huddah Monroe, ameanza kuionesha pete ya uchumba aliyovishwa wiki iliyopita.
Mwanamitindo huyo mwenye umaarufu mkubwa nchini humo, ameamua kuvunja ukimya wake na kuionesha pete hiyo kupitia akaunti yake ya Instagram.
“Kila kitu kipo wazi, lakini muda ukifika watu watamjua nani aliyenivisha pete hii, lakini kwa sasa watu wanatakiwa wajue nina pete ya uchumba.
“Kwa sasa naweza kusema sihitaji usumbufu kutoka kwa mwanamume yeyote, huu ni muda wangu wa kutulia na kufanya maisha na mume wangu mtarajiwa,” alieleza Huddah.
Post a Comment