Wauuguzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala akitoa matibabu kwa wagonjwa wa kipindipindi waliolazwa katika kambi ya hospitali ya Mwananyamala iliyopo manispaa ya Kinondoni jijini Dar es saaam. |
Wauguzi wakiwa katika kambi ya dharura ya kutoa matibabu kwa wagonjwa wa kipindupindu katika hospitali ya rufaa ya Mwanamyamala, Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam. |
Sababu za kuibuka kwa ugonjwa huo zimetajwa kuwa ni kutokana na kutozingatia kanuni za afya huku jamii ikihimizwa kunawa mikono baada ya kujisaidia, kudhibiti ulaji wa ovyo sambamba na kuchemsha maji ya kunywa.
Aidha akizungumza huku akitoa matibabu ya dharura kwa wagonjwa waliopo katika kambi ya mwananyamala Muuguzi wa Hospitali hiyo Eddy Duamo amesema kuwa miongoni mwa dalili za ugonjwa huo unaosambazwa zaidi na Nzi ni kuharisha zaidi ya masaa mawili sambamba na kutapika ambapo imeelezwa kuwa matapishi hayo husambaa zaidi na kuhara kukiwa na hali ya maji ya mchele.
Hata hivyo Mganga mkuu wa manispaa ya kinondoni Dokta Azizi Msuya amesema kuwa hadi sasa kata 70 zimefikiwa na huduma ya dawa sambamba na kupulizia dawa za kuuwa vijidudu vinavyosambaza ugonjwa huo huku ndugu wanaouguza wagonjwa waliopo haspitalini hapo pia wakiwa wamepatiwa dawa kwa ajili ya kuzuia maambukizi zaidi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mussa Natti amesema kuwa hadi sasa hakuna karantini ya kuhudumia wagonjwa hao ambapo hadi iufikia jana jioni maeneo yote yaliyofikiwa na kutokea wagonjwa hao wameshapatiwa dawa ili kuepuka maabukizi zaidi sambamba na kuwataka wakazi wa Wilaya hiyo kutoshiriki chakula cha pamoja na kuepuka kujumuika katika sehemu zenye masonga mano wa watu huku wakishauriwa kuwachunga zaidi watoto kutokana na uelewa mdogo walio nao juu ya maradhi hayo na vihatarishi vyake.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadick amewataka wakazi wote wa Jiji la Dar es salaam kutunza mazingira kwa kuzingatia hali ya usafi, ulaji ulio salama na kuepuka matumizi holela ya vyakula huku akiwata wauzaji wa vyakula na matunda barabarani kuviweka katika hali ya safi na salama kwa kuzingatia kanuni na sheria za afya.
source HS
Post a Comment