0
Msanii wa muziki kutoka kundi la ‘Weusi’ Nikki wa pili, amemnyooshea mikono msanii mwenzake, Jokate Mwegelo, baada ya kufungua njia kwa wasanii na wajasiriamali wapya kama wao katika kufanya biashara na kuzidi kutanua wigo wa biashara yao hususani ya Fashion katika maonesho ya kitaifa.
Akihojiwa redioni Niki wa Pili, amesema kuwa “Kwa sisi kama Weusi kiukweli hatukujianda kwa maonyesho ya sabasaba, halafu pia unajua sabasaba inahitaji uwe na mzigo mkubwa na sisi safari hii hatukuwa na mzigo mkubwa kihivyo na kitu kingine kilitukwamisha kwani mtu ambaye huwa anatufanyia kazi zetu ofisi yake alikuwa ameisimamisha lakini mbali na hilo tulikuwa hatujui namna ya kuweza kupata banda katika maonyesho hayo”.



meongeza kuwa “Lakini kila jambo lina mwanzo tunashukuru Kidoti amefungua mlango kwa sisi wajasiriamali wapya tunaoibukia katika mambo ya Fashion nafikiri mwaka ujao tutajiandaa mapema na kulifanyia kazi na kuitumia hiyo fursa kufanya biashara hiyo, katika plan zetu mwaka huu kiukweli hili suala halikuwepo ila mipango ya mwakani itabidi tuliangalie hili suala maana ni fursa nzuri kibiashara”.
Katika maonesho ya Sabasaba mwaka huu Jokate ndiye msanii pekee ambaye aliweza kuwa na banda la biashara katika maonesho hayo na kuweza kuuza bidhaa zake mbalimbali pamoja na kuweza kujitangaza zaidi.



Post a Comment

 
Top