0
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mama kijacho wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’
Mwanamuziki nchini Tanzania, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na mpenzi wake Zarinah Hassan ‘Zari’ wanadaiwa kuwa hawapo katika maelewano mazuri baada ya mwanamuziki huyo kufunguka kuwa anampenda muigiaji wa Nigeria, Omotola Jalade Ekeinde.
Inadaiwa kuwa kauli hiyo aliyoitoa katika mahojiano na redio moja nchini Nigeria, imezua kizaazaa baada ya wapambe kumfikishia habari hizo mwanadada Zari, na kudai kucharuka vibaya.
Inadaiwa kuwa Zari, anajuata kuwa na Diamond, na inadaiwa kuwa kama usingekuwa ujauzito alionao huenda wangeachana kabisa kwani haiwezekani awe naye kimapenzi na kujitapa hadharani kupenda wanawake wengine.
Kwa mujibu wa mwanamuziki huyo amesema kuwa katika hali ya kawaida kuulizwa swali la mwanamke gani anampenda nchini humo na majibu yalimuelekeza Omotola, Genevieve na Tonto na kama asingewataja angeonekana mbaguzi.
Amedai kuwa anajua kuwa Zari ni mwanamke muelewa sana na anaamini kuwa mambo yatakuwa sawa kwani hawezi kuyumbishwa na maneno ya wambea wa mtandaoni.

Post a Comment

 
Top