0

Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndg Nape Nnauye ametoa ratiba ya Vikao kwa siku ya leo tarehe 10/7/2015:



Saa 4 - 7 mchana.
Kikao cha Usalama na Maadili chini ya M/kiti wake JK.

Saa 8-12 Jioni.
Kikao cha Kamati Kuu kitakachopitisha majina ya wagombea watano.

Baada ya Futar

Saa 2 Usiku:
Kikao cha Halmashauri Kuu kupitisha majina matatu ili Mkutano Mkuu utakaoanza kesho asubuhi upokee majina hayo matatu na kumchagua mmoja wapo atakayepeperusha bendera ya Chama.

SABABU YA KUCHELEWA VIKAO:

Ratiba ya vikao ambayo ilikuwa imetolewa awali haikufuatwa kwa sababu ya Shughuli zilizojitikeza za Mhe Rais za Kichama na Serikali ambazo amekuwa akizifanya tangu alipowasili Dodoma juzi.

Sababu nyingine ni kuwepo kwa Vikao vya mashauriano, ili kuhakikisha kuwa vikao vya mchujo vinaisha kwa salama na hatimae Mgombea wa CCM apatikane kwa Amani.

Post a Comment

 
Top