0
Wabunge wa Tanzania wameishauri serikali kutosaini mkataba wa ushirikiano kiuchumi kati ya umoja wa Ulaya na nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki (EPA) kwa hoja kwamba mkataba huo hauna tija.
7e0685bc-d785-453d-bbc1-a1d6c40edda5_w987_r1_s
Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage,kuwasilisha bungeni mjini Dodoma mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Afrika Mashariki EPA na kuliomba bunge kuishauri serikali.
Ushauri huo umetolewa mjini Dodoma na wabunge wa Bunge hilo baada ya kuujadili mkataba huo kwa kina kwa kutoa maoni yao ambapo wengi wameunga mkono kutosainiwa kwa mkataba huo.
Haya ni baadhi ya maoni ya wabunge kuhusiana na mkataba huo:
Lugola: Kama nchi yetu imekuwa na bidhaa ambazo zimezagaa na kusababisha sisi tusiweze kuimarisha na kujenga viwanda vyetu tukisaini mkataba wa namna hii mheshimiwa mwenyekiti nchi yetu itakuwa ni dampo na bidhaa nyingi za ajabu.
Bashe: Ukiusoma mkataba huu unanikumbusha wakati nasoma form three historia triangular trade,this is another triangular trade in different way ni mkataba ambao unatujenga sisi producers of law materials and become a market.
Ghasia: Mnakwenda kutupangia masharti ambapo tumepigana angalau miaka 50 mnaanza kuweka sera za uchumi,biashara za mapato,sera mbalimbali nzuri inatuambia kwamba tuache sera zote pembeni tufuate masharti ya EU hatukubaliani na hilo.
Lusinde: Yaani huu mkataba kadri unavyousoma kuna sehemu unakuchagulia rafiki wa kufanya naye biashara kuna sehemu unakulazimisha kukaribiana na mtu ambaye kwa wakati huo humuitaji.

Post a Comment

 
Top