Nilipokuwa Lagos, Nigeria, siku mbili kabla ya kufanyika kwa tuzo za Afrima, nilikaa kitako na Diamond Platnumz kuzungumza mambo mbalimbali kuhusu muziki na maisha yake binafsi. Haya ni sehemu ya tuliyozungumza kwenye interview hiyo.
Kuhusu jinsi familia ilivyombadilisha
Nafikiri familia imenifanya niwe nazingatia kile ninachokifanya, nikimaanisha kwamba kuwa makini kwasababu nikifeli sio tu timu yangu bali nafelisha na familia yangu. Kwahiyo nakuwa najitahidi kufanya sababu ya nchi yangu, timu yangu lakini pia mwanangu, kesho na kesho kutwa aweze kuwa proud kusema kwamba ‘baba alifanya hiki na hiki.’ Na kunipa akili ya kuinvest sana sababu usipoinvest usifikiri kwamba unaweza kufika mbali sababu kila mtu anafanya kitu ili kutengeneza msingi bora wa familia yake, vijana wanaokuja isije kubaki story kwamba mtu fulani alivuma sana halafu mwisho wa siku tee.
Kuhusu lugha anayotumia Tiffah kuwasiliana
Ni Kiingereza. Sababu bado hajakuwa katika hatua ya kuongea kabisa lakini maneno yake yote anayozungumza ni ya Kiingereza, hata akisema sitaki, atasema ‘I don’t want it.’ Kwahiyo ndio maana tumempeleka academy ili iwe rahisi sana kwa yeye kuelewa lugha kirahisi kwasababu pale nyumbani kwao wanazungumza mpaka Kiganda, kuna Kiswahili kidogo, kuna Kiingereza kwahiyo inaweza ikamchukua hata miaka mitano hadi ashike vitu vyote, lakini kwenye academy wanafundisha Kiingereza tu, inakuwa rahisi kwake kuzungumza Kiingereza.
Kuhusu lugha anayotumia anapokuwa anazungumza na Zari
Kiingereza. Kadri siku zinavyokwenda anakuwa anakielewa Kiswahili, nafikiri kwasababu ndio maana hata mkiongea Kiingereza kiasi gani lakini lugha ya kwenu itabaki kuwa ya kwenu. So tunaongeza, sometimes ananiskia mimi na familia tunaongeza Kiswahili, sometimes namfundisha maneno ya Kiswahili lakini pia mwenyewe ni mwepesi na hata mkikutana naye anakielewa Kiswahili hapo si sana.
Kuhusu tetesi za kumsaliti Zari
Kitu ambacho niko proud sana ni mpenzi wangu mimi ni mwelewa sana, na tangia tunaanzana anaelewa kwamba mimi ni maarufu, yeye ni maarufu. Mimi nitasikia vitu kwake, yeye atasikia vitu kwangu, ni staa nakaa Tanzania, of course ni mtu ambaye nikiwinda siwezi kukosa au kuna mtu anaweza kuniwinda kinamna yoyote.
Lakini mwisho wa siku ni ufahamu wangu mimi kuwa mwanaume na ni namna gani naweza kumheshimu mwenzangu, kuweza kumpenda mwenzangu, naweza kumlindia heshima yake, anajikinga vipi na hivyo vitu vibaki kuwa story na sio vitu vya kweli kwasababu kusema vitasemwa tu. There is no way simba akapita katika zizi la swala akaondoka watu wakasema hakula swala hata mmoja, watasema tu alikula hata kama hakula.
Bongo5

Post a Comment