0
Kufuatia skendo ya utapeli inayoendelea kumwandama mwimbaji wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando anadaiwa kupigwa pingu mkoani Dodoma, baadaye akasafirishwa hadi Dar kwa msimamizi wa kazi zake, Alex Msama, kwa lengo la kumlipia deni alilokuwa akidaiwa. Habari kutoka kwa chanzo zimeeleza kwamba, hivi karibuni, Rose alilipwa Sh. milioni 3 kwa ajili ya shoo huko Makambako mkoani Njombe na matangazo yakafanyika lakini hakutokea. Ikadaiwa kuwa, wakati matangazo ya shoo yakiendelea, mtu mwingine aliyekuwa akimdai Sh. milioni 3.5 (pia alichukua fedha kwa shoo siku za nyuma) alikwenda Makambako kwa lengo la kumsubiri Rose ili amnase, lakini hakutokea. Chanzo hicho kiliendelea kumwaga ‘unyunyuzi’ kuwa, wawili hao waliripoti ishu ya Rose, Kituo cha Polisi Makambako ambapo polisi walifunga safari kumfuata Dodoma. Sosi huyo alisema kuwa, Rose alikamatwa Juni 27, mwaka huu na kuswekwa rumande Kituo Kikuu cha Polisi, Dodoma tayari kwa kupelekwa mahakamani. Imedaiwa kuwa, kigogo mmoja wa serikali mkoani humo (jina lipo) aliwaambia polisi wampigie simu Msama na kumweleza kisanga hicho ili ikibidi yeye amlipie deni hilo kwa sababu anamsimamia kazi zake. “Msama alikubali kwa sharti kwamba, kwa sababu ana kazi ya kufanya na Rose hivyo asafirishwe hadi Dar amlimpie, yeye na Rose watakatana kwenye kazi. “Rose alisafirishwa Juni 29, mwaka huu akiwa chini ya ulinzi wa askari wawili. Mmoja wa kike ambaye alilala naye chumba kimoja hotelini. Kesho yake wakaenda ofisini kwa Msama, Block 41, Kinondoni, akalipa milioni sita na laki tano keshi,” kilisema chanzo.

Post a Comment

 
Top