0
Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Hamad Masauni amesema kuwa serikali imewafukuza askari polisi 152 kwa makosa ya utovu wa nidhamu kuanzia Juni 2015/2016.
4-3
Akizungumza Naibu waziri wa Mambo ya Ndani Jumatatu hii, akiwa bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu, Mariam Sabaha,lililohoji,Je? “serikali imewachukulia hatua gani askari polisi wanaobainika kuwapiga raia bila makosa?”, waziri Masauni ametoa ufafanuzi
“Jeshi la Polisi hufanya kazi kwa mujibu wa sheria, linazingatia kanuni na taratibu zilizopo hata hivyo askari wachache ambao wamekuwa wakikiuka maadili ya mwenendo mwema wa jeshi la polisi kama ambavyo imeanishwa katika kanuni za kudumu za polisi namba 103,”amesema Masauni.
“Serikali kupitia jeshi la polisi limekuwa likichukua hatua mbalimbali za kinidhamu kwa watumishi wanaoonekana kwenda kinyume na maadili ya kazi za jeshi la polisi,ikiwemo kuwapiga wananchi wasio na hatia,matharani kuanzia kipindi cha mwaka 2015/2016 Juni askari 200 walichukuliwa hatua za kinidhamu, muheshimiwa mwenyekiti jumla ya askari 152 walikutwa na hatia na kufukuzwa kazi,”ameongeza.

Post a Comment

 
Top