Jeshi
la Polisi Mkoani Mwanza limewafukuza kazi askari watatu kwa tuhuma za
kukiuka maadili ya kazi ikiwemo kujihusisha na vitendo vya utovu wa
nidhamu pamoja na upokeaji wa rushwa.
Akizungumza
na askari hao Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema
kuwa hatua imechukuliwa ili iwe fundisho kwa askari wengine wanaokwenda
kinyume na maadili ya kazi hiyo.
Amesema
askari mmoja kati ya hao alikutwa akiwa amelewa na kulala lindoni, huku
wengine wawili wakituhumiwa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.
Kamanda
Msanga amesema ukiukwaji wa maadili ni chanzo cha ongezeko la uhalifu
hivyo hatamvumilia askari yoyote atakaye kwenda kinyume kwa kuwa kwa
kufanya hivyo kunalichafulia hadhi jeshi la polisi kwa sababu ya makosa
ya askari wachache.
Post a Comment