0



Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ametoa onyo kwa watu watakaoandamana bila vibali, huku akiwataka vijana kutofuata mkumbo.
nchemba1
Nchemba ametoa kauli hiyo kwenye mahojiano maalumu katika kipindi cha HOT MIX kinachorushwa na EATV kuhusu msimamo wa vyombo vya usalama nchini kutokana na kuwepo kwa kauli mbalimbali wa vyombo vya siasa vya kutangaza kuwepo na maandamano ya amani.
“Kwanza wasifuate mkumbo, kwenye vitu ambavyo vimekatazwa na ni sheria wasikiuke sheria, wasifanye kiburi, kwasababu yule atakayeenda kinyume na sheria na atakayekiuka atafikishwa katika mkono wa sheria, lakini kwa yule anayefanya kazi bila kuvunja sheria atapata ulinzi kuhakikisha kuwa anakuwa salama na anafanya kazi kwa usalama”, alisema Nchemba

Post a Comment

 
Top