0

BASATA lawataka wasanii kuhakikisha wamesajiliwa na kuwa na vibali vya Baraza, laonya mapromota watakaotumia wasanii wasiosajiliwa.

Wakuzaji sanaa wote (Mapromota) wanaoendesha matukio ya Sanaa kama vile matamasha, mashindano, maonyesho na utoaji tuzo nchini kuhakikisha wanafanya kazi na Wasanii waliosajiliwa na wenye vibali vya BASATA na si vinginevyo.

Sambamba na hili, BASATA linawaagiza wamiliki wote wa studio (Production Houses) zinazozalisha kazi za Sanaa kuzisajili mara moja na kuhakikisha zinakuwa na vibali halali vya Baraza la Sanaa la Taifa.

Post a Comment

 
Top