0
Nay wa Mitego hana msichana mpya wa kumuita ‘Valentine’s’ wake ndio maana aliamua kumchagua Ex wake, Shamsa Ford kwenye siku hiyo iliyoadhimishwa Jumapili iliyomalizika.
Tatizo ni kuwa, Shamsa yupo mikononi mwa mwanaume mwingine na hajapenda salamu za Nay kwenye Instagram alikompost.
“Naona mambo yanazidi kuvumishwa kwamba nimerudiana na Nay. Pls pls nina maisha yangu na mwanaume ambae nampenda na kumuheshimu. ..sijarudiana na nay na haiwezi kutokea kabisaaa,” aliandika Shamsa.
“Nay una ndugu na marafiki wengi wa kuwaposti siku ya leo haikuwa muhimu uniposti mimi.nilishukuru Mungu watu walishasahau kuhusu mimi na ww but naona umetaka kuyafufua. Sipendi scandal na si maisha yangu kutafuta kiki za kijinga. KAZI YANGU NDO INAYONITAMBULISHA. ..PLS TUESHIMIANE,” aliongeza.
Shamsa Ford na Nay walikuwa na uhusiano wa kimapenzi uliodumu kwa muda mfupi.

Post a Comment

 
Top