0
IKIWA imepita siku moja toka taasisi ya kupambana na Rushwa TAKUKURU kupitia kwa naibu mkurugenzi mkuu wake Valentino Mlowola kutangaza kuwa hadi kufikia sasa taasisi hiyo imefikisha mahakamani jumla ya kesi 36,Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe ameijia juu taasisi  hiyo kwa kushindwa kuichukulia hatua kampuni ya mafuta ya Like Oil ambayo inatuhumiwa kukwepa kodi.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Zitto ameandika hivi.

"Nimesoma taarifa ya ‪#‎TAKUKURU‬ kuhusu kesi zaidi ya 30 na mashauri 4 mazito yanayopelekwa mahakamani hivi karibuni. LakeOil anatuhumiwa kukwepa kodi tshs 8 bilioni na kupewa miezi 2 walipe. IPTL/PAP inalipwa kila mwezi 8 bilioni na #TAKUKURU wameufyata kueleza umma hatua wanazochukua. Miezi 3 sasa toka Magufuli aingie madarakani, Harbinder Singh Seth keshavuta tshs 24 bilioni. Kama kawaida tunaanza kuona PR work ya vipaza sauti wa IPTL/PAP wakipewa kurasa za mbele za magazeti makubwa na yenye heshima nchini. Usaha wa jipu la IPTL unanuka"

Post a Comment

 
Top