0
Hatimaye Baraka Da Prince ameweka wazi kuwa hakuna uhusiano wowote wa kimapenzi na Staa wa Bongo Movie Nisha ila mashabiki ndiyo wanakuza mambo.

Baraka amesikika kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Afrika Radio,  akisema yeye na Bi dada ni washikaji tu na wamekuwa wakionekana sehemu mbalimbali pamoja ndiyo maana watu wanasema ni wapenzi.

“Siko kwenye mahusiano offcorse na hata kama ningekuwa kwenye mahusiano sijawa  tayari kuzungumzia mahusiano yangu”

Alisema Baraka na kuongeza
“Nisha Mimi ni rafiki yangu bana,ni mtu ambaye nipo naye muda mwingi,hivyo sina mahusiano yoyote na Nisha”

Ameongeza pia kuwa Watu wamekuwa wakimpakazia mara kibao kuwa ana mahusiano na Watu wakati si Kweli, Baadhi ya wasichana baraka aliowahi kutajwa kuwa nao kwenye mahusiano ni Agness Masogange na Menina.

Post a Comment

 
Top