Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’. |
Chanzo makini kimeeleza kuwa, miezi kadhaa iliyopita, Steve alimpeleka rafiki yake aitwaye Mohamed maarufu kwa jina la Mo kwa tajiri wake (jina tunalihifadhi) kisha akamtambulisha kuwa anafanya shuguli za kuuza na kutengeneza magari ndipo Mo alipotumia mwanya huo kuchukua fedha na kumzungusha tajiri huyo.
- “Tajiri alivyotambulishwa na Steve kwamba Mo ni rafiki yake, wakabadilishana namba za simu na ndipo siku moja huyo tajiri akampa Mo dili la kutengeneza gari yake iliyokuwa imegongwa kwa shilingi milioni 13, Mo akachukua hela lakini kila akiulizwa lini gari itatoa, hatoi majibu.
- “Akawa anapiga chenga, mara niko Sauz mara niko wapi. Sasa huwezi amini tajiri akahisi Steve naye amehusika. Ikabidi ampeleke Polisi Oystebay, akahenyeshwa kwelikweli ili aeleze ukweli anavyomfahamu Mo lakini bahati nzuri akaachiwa baada ya polisi kujidhirisha,” kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa Steve kuhusiana na tukio hilo, hakutaka kufafanua kwa undani zaidi akamuomba mwandishi wetu aachane nalo akidai ‘soo’ hilo wameshalimaliza Mo na huyo tajiri.
“Mi naomba tu uachane nayo hiyo ishu, wameshamalizana wenyewe, lipotezee,” alisema Steve na kukata simu.
Post a Comment