0
Msanii mkongwe wa filamu Dk Cheni amedai ameamua kuacha kufanya filamu kwa muda mpaka pale soko la filamu litakapo kuwa sawa.
Dr Cheni
Mwigizaji huyo ambaye amekuwa na mchango mkubwa katika tasnia ya filamu hasa hasa kuinua vipaji vipya vya uigizaji, ameitaka serikali kuweka mazingira mazuri ambayo yatalinda kazi za wasanii.
“Kusema kweli hali ni mbaya sana,” Dr Cheni alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV. “Binafsi kwa sasa nakaa pembeni kwenye masuala ya filamu mpaka soko litakapokuwa sawa,”
Aliongeza, “Wezi wa kazi za wasanii ni tatizo sugu kwetu. Kwa hiyo mimi niseme tu serikali inatakiwa kuangalia kwa makini suala hili hasa hasa kudhibiti maharamia wa kazi za wasanii,”
Dk Cheni amedai wanaosambaza kazi zao ndiyo wezi wa kazi zao japokuwa taarifa zinaweza zikawa hazijaifikia serikali lakini watajitahidi kutoa ushirikiano kwa Mh.Nape Nnauye ili kuweza kuwakamata wezi kirahisi zaidi na kuokoa tasnia hii.

Post a Comment

 
Top