0
Sababu za kwako kumzimia mwanamke ambaye tayari ana boyfriend sizijui ni zipi. Labda ulikuwa umemzimia tangu zamani lakini ulikosa mbinu za kumtongoza akachukuliwa, labda unataka kulipiza kisasi, ama labda unaona huyo boyfriend aliye naye sahizi hafai...ama sababu tofauti kabisa na hizi. Well, jawabu langu ni kuwa, hakuna chochote kisichowezekana hapa ulimwenguni. Mwanzo inaweza kuwa rahisi zaidi kumnyakua mwanamke huyo bila wewe kutoamini. Kile unachohitajika sasa nikufuata hizi mbinu ambazo zimehakikishwa na kufanyiwa utafiti.

1. Kuwa mwanaume ambaye anakuwa kwa ndoto ya kila mwanamke
Kuwa na tabia za kigentleman. Kuwa gentleman itamfanya mwanamke yeyote yule akuwaze na kukutia ndotoni mwake na pia kutaka kukujua zaidi ama atleast kuwa mnakutana mara kwa mara. Hakikisha pia kando na kuwa na tabia za ugentleman, hakikisha ya kuwa unapenda kuwa karibu na yeye na akianza kuonyesha dalili zozote zile, mfano kukupa busu kipajini au kwa shavu, ama kupenda kukukumbatia, fahamu kuwa unaenda sambamba na ajenda yako. Pia kumfanya akuweke kwa akili yake lazima uonyeshe interest zako kwake.

2. Usiache kumuangalia
Wakati ambapo mnakuwa pamoja mnaongea, hakikisha kuwa macho yako yote yanamuangalia yeye kila wakati. Hii ni ishara ambayo itamuonyesha yeye kuwa una macho ambayo yanamzimia yeye pekeake. Mbinu hii itamfanya kwa urahisi kutaka kukutia machoni akuangalie kama bado tabia ya kumuangalia yeye uko nayo ama la.

3. Usisahau kutumia lugha za kumsifu
Ukweli usemwe. Watu wakiwa katika mahusiano kwa muda mrefu kuna vitu mbavyo wanavichukulia kama mzaha. Mfano katika mahusiano ya mwanamke na mwanamume, unapata mara nyingi wamezoeana kiasi cha kuwa wanajihisi uhusiano wao umeshikana kiasi cha kuwa wanasahau mambo madogo madogo kama vile kumsifu mpenzi wake, kumzawadi nk.
Hii ni njia wapo rahisi ambayo itakuwezesha wewe kuuteka moyo wa mwanamke ambaye ana boyfriend kwa haraka. Maneno ya kumsifu ambayo hajaambiwa kitambo yanaweza kumchanganya akili mwanamke yeyote na kumfanya kuingiwa na hisia mbili mbili. Niamini ukitumia mbinu hii utakuwa na nafasi kubwa ya kwako kufaulu kumpata mwanamke aina hii.

4. Hakikisha umemuelewa ndani na nje
Wengi wangeuliza itakuwaje kumfahamu mwanamke ndani na nje na tayari ana boyfriend? Kama ulikuwa hujui basi ni hivi, kulingana na utafiti, inasemekana kuwa akili ya mwanamke inafanya kazi tofauti kabisa na ya mwanamume. So usitilie shaka kabisa hapa. Pia hakikisha umesikiliza kila kitu ambacho atakwambia na utilie maanani yote atakayosema.

KUMBUKA: Wanawake hujiskia huyu kuongea yote ambayo yanatoka akilini mwao kwa mwanamume ambaye anamuamini na kumkubali. Hivyo ukiona umefikia level hii fahamu ya kuwa hauko mbali na kutimiza lengo lako kuu. Pia usisahau kutumia maneno ya uchezi ili kupunguza tenshen ambayo inaweza kuwa kati yenu.

ONYO: Usijaribu kumwambia moja kwa moja kuwa unamzimia na unataka kumpokonya kutoka kwa boyfriend wake kwa sababu hio haitafanya kazi kamwe.

Post a Comment

 
Top