0
Msanii wa filamu na mwanamuziki nchini Tanzania, Flora Mvungi
Msanii wa fiamu nchini Tanzaia, Flora Mvungi ‘H-Mama’ amewashangaa watu wanaomsema pembeni kuwa amewahi kuchepuka na kukanusha vikali kuwa hakuwahi kufanya hivyo tangu afunge ndoa na mumewe, Khamisi Ramadhani ’H-Baba.’
Amedai kuwa tangu wakutane na H-Baba, kipindi cha uchumba wao hajawahi kumsaliti hata siku moja zaidi ya kudumisha uaminifu mpaka leo na kuwashangaa watu kusema mambo wasiojua undani wake.
Ameongeza kuwa anakasirishwa sana na watu ambao kazi yao ni kusema ya watu na kudai kuwa kuchepuka anachukia katika maisha yake na kusema kuwa anafurahia sana maisha ya ndoa pia namshukuru Mungu kwa kubahatika kupata watoto wawili Tanzanite na  Afrika.
Sambamba na hilo amesema kuwa wanawake wengi wanakosa uvumilivu na kusababisha ndoa zao kuvunjika kutokana na tamaa na kuwataka kuheshimu ndoa zao na wasifanye ndoa kama fasheni

Post a Comment

 
Top