0



Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt John  Pombe Magufuli jana  alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa  Dar  es Salaam, Paul Makonda kwa juhudi anazofanya katika ziara yake kwa kusikiliza kero za wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Rais Dkt Magufuli alitoa pongezi hizo alipompigia simu Mkuu wa Mkoa wakati akiwa katika ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi katika maeneno ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

“Endelea hivyo kutembelea wananchi na kutoa ufafanuzi kwa sababu nyingine ufafanuzi huu kama ungetolewa mapema wala wananchi wasingekuwa na sababu ya kuja kuuliza maswali kui kwa hiyo endeleeni hivyo hivyo na juhudi za Dar es Salaam na wakuu wa Wilaya yako na watendaji wote kwa kazi nzuri mnazozifanya kwa kusikiliza kero zao bila kujali vyama vyao bila kujali makabila yao na uendelee kutumbua huko huko” alisema Rais Magufuli.

Hapa chini ni sauti ya Rais Magufuli akitolea ufafanuzi suala la upanuzi wa barabara

Post a Comment

 
Top