0




Hatimaye  rufaa ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema iliyokatwa na mawakili wake itasikilizwa Jumatatu ijayo.

Rufaa hiyo itasikilizwa na Jaji Fatma Masengi ya kuomba mbunge huyo kupewa dhamana baada ya mawakili wanaomtetea jana kusajili maombi ya rufaa namba 112/113 ya mwaka 2016 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, ili kudai haki ya dhamana ya Lema aliyonyimwa kutokana na makosa ya kisheria yaliyofanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Rufaa hiyo imepokewa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha na kupangwa kwa Jaji Masengi ambaye ndiye atakayeamua hatma ya Lema kuwa nje kwa dhamana au la.

Mawakili wa Lema  ambao ni Sheck Mfinanga na Peter Kibatala jana walisema tayari wamesajili rufaa yao Mahakama Kuu na wanasubiri siku hiyo ili isikilizwe.

Mfinanga alisema wameamua kufungua maombi ya rufaa kwa ajili ya kujua ni kwa nini Lema amekosa dhamana ambayo awali Hakimu Desdery Kamugisha alisema ipo wazi.

Post a Comment

 
Top