0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa amri kukamatwa kwa mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu na kuamuru wadhamini wake kufika mahakamani hapo.
lissu
Amri hiyo imetolewa na Hakimu Thomas Simba baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa kesi yake ilipangwa kusikilizwa Alhamisi hii lakini Lissu hakuwepo mahakamani hapo.
Alijitokeza mdhamini wake mmoja kati ya wawili, Robert Katula na kudai kuwa mshtakiwa huyo anaendesha kesi ya uchaguzi wa mahakama kuu Tanzania kanda ya ziwa.
Hakimu alimhoji mdhamini huyo kwanini mshtakiwa amesafiri na kuacha kuhudhuria kesi yake bila kuomba kibali cha mahakama yake.
“Mshtakiwa Lissu anafanya dharau kila anapopangiwa kesi yake mahakamani anashindwa kuhudhuria bila kutoa sababu wala kuomba ruhusa ya mahakama, kama asingekuwa nje kwa dhamana angefanyaje”?alihoji. “Angetumia busara kuomba ruhusa.”
Wakili wa serikali Patrick Mwita aliomba mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa mshtakiwa.

Post a Comment

 
Top