0
Rapper Roma Mkatoliki amefunguka juu ya mipango yake ya kufanya collabo na wasanii wa mataifa mengine kama walivyofanya baadhi ya wasanii wengine wa Hip Hop Bongo akiwemo Joh Makini na Fid Q.
14718416_1154125078000548_447783841352908800_n
Roma amemuambia mtangazaji wa Maisha FM ya Dodoma, Silver Touchez “Kufanya collabo na wasanii wa mataifa mengine inakuza muziki wako lakini pia na profile yako inakuwa kwa kuwa unakuwa unatambulika kwenye hiyo nchi nyingine.”
“Ni ngumu kukwambia ninavyopambana kuwa nilikuwa naongea na fulani nataka nipige naye collabo, lakini kila kitu kitakapo kuwa kwenye mstari watashuhudia tu kwa sababu it’s a matter of network na connection tu hakuna uchawi mwingine,” ameongeza.
Katika hatua nyingine msanii huyo amewapongeza rapper wa Bongo ambao tayari wameshafanikiwa kufanya collabo na wasanii wa nje.

Post a Comment

 
Top