Upande
wa Jamhuri kwenye kesi ya Salim Njwete maarufu kama 'Scorpion'
anayetuhumiwa kumwibia Saidi Mrisho na kumtoboa macho kwa kisu umedai
mahakamani hapo kwamba upelelezi haujakamilika na kuomba siku nyingine
ya kukamilisha.
Mshitakiwa Njwete 34, anashitakiwa kwa kumwibia Mrisho na kumjeruhi kwa kumchoma tumboni, mabegani na machoni.
Taarifa
ya upelelezi kutokamilika ilielezwa jana na Mwendesha Mashitaka
Chensensi Gavyole mbele ya Hakimu Mkazi Flora Haule kesi hiyo ilipotajwa
na kuangaliwa kama upelelezi umekamilika.
“Mshitakiwa
yuko mbele ya Mahakama hii lakini upelelezi haujakamilika, tunaomba
Mahakama itupangie siku nyingine ya kutajwa kutokana na upelelezi
kuendelea,” alisema Gavyole.
Kutokana na sababu hizo, Hakimu Haule aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 16 itakapotajwa tena.
Mshitakiwa
huyo maarufu kama Scorpion alifikishwa mahakamani hapo akiwa kwenye
gari dogo la mizigo tofauti na siku za nyuma ambapo alikuwa akiletwa
akiwa kwenye basi la Magereza.
Awali
ilidaiwa kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 9 Buguruni Sheli
alipomwibia Mrisho fedha na vitu vyenye thamani ya Sh 476,000 na
kumjeruhi kwa kumchoma kisu tumboni, mabegani na machoni.
Post a Comment