0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewashukuru viongozi wa dini nchini kwa kuendelea kuliombea taifa amani.
a14
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akimpatia Charles Mang’enya shilingi milioni kama zawadi kwa vikundi vya kwaya vya kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano jijini Dar es salaam
Ametoa shukrani hizo jijini Dar es Salaam aliposhiriki ibada ya Jumapili katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano, lililopo Posta, jijini Dar es Salaam.
a4
Rais Magufuli na mkewe Bi. Janet wakifuatilia misa
“Ninawashukuru kwasababu mnaendelea kuliombea taifa hili, ninawashukuru kwasababu siku zote mmekuwa mkipiga goti kwaajili ya kumtanguliza Mungu mbele, ninawashukuru kwasababu mnandelea kuiombea amani ya nchi yetu na upendo udumu ndani yetu sisi wote makanisa yote, madhehebu yote, dini zote, vyama vyote, upendo tukiujenga ndiyo tutaiendeleza vizuri Tanzania yetu,” alisema Dkt Magufuli.

Rais Magufuli akisalimiana na waumini wa kanisa hilo
Rais Magufuli akisalimiana na waumini wa kanisa hilo
“Napenda nichukue fursa hii kwasababu ni mara yangu ya kwanza kufika hapa, kwa niaba ya wakristo wote wa Anglikana, napenda niwashukuru sana kwa kura nyingi mlizonipa ambazo zimenifanya mimi nikawe rais. Ni kazi ngumu, inahitaji kumtanguliza Mungu, endeleeni kutuombea ili tufike mbele tuweze kuyatimiza haya tuliyoyaahidi kwa wananchi na haya ya kuiweka Tanzania ya umoja,amani na upendo miongoni mwetu lakini Tanzania yenye maendeleo,” aliongeza.
Hizi ni picha zingine:

a22
Rais Magufuli akisalimiana na waumini wengine wa kanisa hilo mara baada ya misa
a24
Rais Magufuli akiwapungia mkono waumini wa kanisa Anglikana la Mtakatifu Albano baada ya kumalizika kwa misa
a26 a27

Post a Comment

 
Top