0
Bushoke ni miongoni mwa waimbaji na watumbuizaji wazuri waliowahi kukamata chati nyingi za muziki miaka kadhaa iliyopita kupitia hits zake mbalimbali ukiwemo ‘Mume Bwege.’
bushoke-mpita-njia
Hivi karibuni ameachia wimbo wake mpya uitwao ‘Mpitanjia’ unafanya vizuri kwa sasa.
Akiongea na mtangazaji wa ABM Radio ya Dodoma, Dj Rodger, Bushoke amesema alikuwa na wazo la wimbo huo miaka minne iliyopita na alipata wazo hilo alivyokuwa Uganda.
“Unajua huu wimbo umekaa sana studio na nilikuwa na idea ya wimbo huu kichwani zaidi ya miaka minne tokea nipo Uganda,” alisema. “Mpitanjia ni kipande ambacho kiliimbwa na Mbaraka Mwishehe na kipande hicho nilikipenda sana na ndio maana nikaamua kuanza nacho, na nilitaka kukipa heshima zaidi, najua watu wengi huo wimbo hawaufahamu na mara ya kwanza umekamilika huu wimbo nikiwa South Africa nilikuwa naupiga kwenye keyboard.”
mbaraka-mwishee
Bushoke aliongeza kuwa aliufanya tena wimbo huo Dodoma.
“Niliufanya kwa mara ya kwanza Dodoma kwa Silas, sasa nilikuwa kila nikitaka kuumaliza Silas alikuwa busy nikaona bora niurudie tena kwa Ema the Boy ila nikaona kama bado nikamtafuta tena Allan Mapigo naye akapiga vya kwake. Kwahiyo ni wimbo ambao umekaa muda mrefu sana studio ila kuna watu ambao wakiisikia hiyo ambayo nimefanya Dodoma wanasema hiyo kali zaidi sasa nitakachofanya, nitaifanyia remix hapo baadaye,” alieleza Bushoke.

Post a Comment

 
Top