Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira Luhaga Mpina amesema umefika wakati wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu kuangalia upya sera ya ukopeshaji ili waweze kutoka mikopo kwa ngazi ya Astashada kwa masomo ya Sayansi ili kupata wataalam wengi wa fani hiyo
Mhe. Mpina amesema kuwa hatua hiyo itawezesha kwenda sambamba ma mapinduzi ya maendeleo ya uchumi wa viwanda jambo ambalo litawezesha taifa kuwa na wataalam wengi wa mambo ya Sayansi na kuongeza tija katika ustawi wa maendeleo ya viwanda.
Akiongea na uongozi wa juu wa bodi ya mikopo ya elimu ya Visiwani Zanzibar, amesema Tanzania sasa inataka kuingia katika uchumi wa viwanda jambo ambalo linahitaji wataalam wengi wa masomo ya Sayansi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo Tanzania, Abdul-Razaq Bandru, amesema kuwa bodi hiyo inafanya marekebisho mbalimbali ikiwemo kufanikisha mabadiliko ya kanzidata ili kuwafikia wadaiwa kwa urahisi zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Luhaga ametoa pongezi kwa tume ya taifa ya nguvu za atomic visiwani Zanzibar na kuwambia kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuimarisha na kuisimamia ofisi za tume hiyo visiwani Zanzibar.
Post a Comment