0

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ( Chadema) anayeshikiliwa katika mahabusu ya kituo kikuu cha Arusha Mjini amegoma kula kwa zaidi ya saa 48 sasa tangu alipokamatwa

Lema alikamatwa juzi alfajiri akiwa nyumbani kwake Njiro Arusha kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi  na kushawishi watu kwa njia ya mtandao waandamane Septemba mosi.

Jana Meya wa Arusha, Calist Bukhay alisema Lema amegoma kula

Alisema Lema aligoma kula akidai kuwa alifanyiwa udhalilishaji mbele ya watoto wake wakati polisi walipokuwa wakitekeleza agizo la kumkamata.

"Ni kweli amegoma kula tangu jana (juzi) alipokamatwa.Alisema askari polisi walipkwenda kumkamata walimfanyia vitendo vya udhalilishaji mbele ya watoto wake na kumnyanyasa bila kujali yeye ni kiongozi wa wananchi.

"Sasa  yeye ameshikilia msimamo wake kuwa kwa kuwa polisi walikuwa wamepanga kumuua wakati wa kumkamata, basi ni bora akafa kwa njaa.

"Chakula kimekuwa kikipikwa na kupelekwa na mkewe ,lakini bado amegoma kukila.Baada ya tukio hilo, polisi walituita ili kujaribu kumshawishi ale mchana, akagoma" Alisema Meya Calist

Post a Comment

 
Top