Jeshi la Polisi Kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam limekusanya shilingi milioni 320.2 ambapo fedha hizo ni kutokana na tozo za makosa ya usalama barabarani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam Kamanda wa wa polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema fedha hizo ni kutokana na makosa 10,676 ambayo yamefanywa na watumiaji wa vyombo vya moto.
‘’Toka tarehe 25 hadi tarehe 28 tumefanikiwa kukusanya kiasi nilichotaja ambapo makosa mengi ya madereva wa bodaboda tumeanza kuona kwamba tunapowatoza faini ya elfu 30 au 60 haiwapi fundisho lolote ndiyo maana tumekuwa tukiwapeleka mahakamani ili kupunguza matukio ya uvunjifu wa sheria barabarani’’ Alisema Kamanda Sirro
Aidha Kamishna Sirro alitumia wasaa huo kuwataka watanzania kutii sheria bila shurti wanapokuwa wanatumia vyombo vya moto barabarani na katika maeneo yao ya kuishi.
Post a Comment