0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jana  July 29 2016 alianza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma ambapo alizungumza na wananchi kwa lengo la kuwashukuru kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kueleza juhudi zinazofanywa na serikali katika kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo.

Akizungumza na wananchi wa Manyoni mkoani Singida Rais Magufuli alizungumzia kuhusu wabunge wa upinzani kususia bunge  kwa kujiziba  midomo na makaratasi 
Alisema wabunge hao wa upinzani waliamua kususia  bunge kwa sababu kilichokuwa kikijadiliwa ndani ya bunge ni mahakama ya mafisadi na wao (wapinzani)  ni sehemu ya mafisadi .
"Hawakuingia kwenye bunge kwa sababu walijua ni part ya hao mafisadi, nataka nieleze hawatapenya mbele ya serikali yangu, mafisadi lazima wanyooke" Alisema Rais Magufuli

Post a Comment

 
Top