Septemba Mosi, 2015 Tanzania ilianza kutumia sheria ya Makosa ya Mtandao licha ya kuwepo kwa mvutano na malalamiko kutoka kwa wananchi wanaotumia mitandao hiyo kwamba hawakushirikishwa kuijadili na kuichambua.
Leo March 4 2016 Kampuni ya Jamii Media inayoendesha JamiiForums.com na Fikrapevu.com imejitosa kutetea kile inachokiita ni kunyimwa haki ya wananchi kupata taarifa na kulindwa kwa uhuru wao wa maoni na kujieleza unaolindwa kwa mujibu wa katiba ya Nchi.
Jamii Media wameamua kufungua shauri Mahakama kuu kutaka kifungu cha 32 na 38 cha sheria ya Makosa ya Mtandao viangaliwe upya. Akizungumza kwa niaba ya Jamii Media,wakili Shukuru Mlwafu ameeleza…
"Baadhi ya vifungu vya sheria ya kimtandao vinakiuka masharti ambayo yamewekwa na katiba hasahasa vinaingilia haki ya faragha ambayo wateja wetu wanayo kikatiba.
"Njia pekee ni kufungua shauri la kikatiba kupinga vifungu hivyo na kuiomba mahakama ibatilishe na itamke kuwa vifungu hivyo ni batili kwa kuwa vinaenda kinyume na ibara 16 na 18 ya katiba" Amesema Shukuru Mlwafu
Hatua hiyo ya kufungua shauri Mahakamani imekuja baada ya kuwepo na shinikizo kutoka Jeshi la polisi kuwataka Jamii Forum kutoa taarifa za baadhi ya wateja wake. Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Maxence Melo amesema..
"Kuanzia uchaguzi october 2015 kumekuwa na barua kadha wa kadha zinazotaka kupata taarifa za siri za wanachama wa mtandao wa jamii forum kitu ambacho tunahisi hata mitandao mingine ya kijamii wanafanyiwa na kumekuwa na mashinikizo kadha wakadha wakitaka tutoe IP Address za wateja, majina halisi na hata maeneo waliopo.Sasa tunaona hii itapekea kuvunjwa kwa haki ya watumiaji wa Jamii forum":-Amesema Maxence Melo

Post a Comment