0
baadhi ya magari yaliyokuwepo hotelini hapo yaliyoharibiwa vibaya
Waziri wa usalama wa ndani nchini Somalia amesema watu 20 walifariki baada ya hoteli mbili maarufu za ufukweni kushambuliwa mjini Mogadishu.
  • Bw Abdirisak Omar Mohamed ameambia idhaa ya Kisomali ya BBC kwamba watu wengine 20 walijeruhiwa baada ya hoteli za Lido Sea Food na Beach View kushambuliwa Alhamisi jioni.
  • Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la al-Shabaab limedai kuhusika kwenye shambulio hilo.
Mabomu yaliyotegwa kwenye magari yalilipuka kabla ya wapiganaji kuingia hotelini na kuanza kufyatulia watu risasi.
zaidi ya watu 20 walipoteza maisha kwenye tukio hili
Wapiganaji hao waliwashikilia mateka wageni na wafanyakazi wa hoteli kwa muda wa saa nane.

Maafisa wa serikali ya Somalia wamesema kwa sasa maafisa wa usalama wamefanikiwa kuchukua udhibiti wa hoteli hizo na mhusika mkuu wa shambulio hilo amekamatwa.

Waziri mkuu wa Somalia, Omar Abdirashid Ali Sharmarke, ameshutumu mashambulio hayo na kuyataka kuwa ya “kikatili”.

Post a Comment

 
Top