0
rose mhando
DAR ES SALAAM! MAJARIBU! Staa anayefanya vizuri kwenye Muziki wa Injili Bongo, Rose Muhando yupo hoi kitandani baada ya kung’atwa na nyoka.

Chanzo makini kililiambia gazeti hili kwamba Rose akiwa anaingia getini usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita, nyumbani kwake mkoani Dodoma aling’atwa na nyoka mguuni na kukimbizwa hospitali iliyopo Area C mkoani humo.


  • “Maskini Rose ana majanga sana kwa kweli maana alikuwa bado hajapona ule ugonjwa wa kuvimba miguu na mikono lakini amejikuta katika wakati mgumu tena baada ya kung’atwa na nyoka nyumbani kwake,” kilisema chanzo hicho.


Baada ya kuzipata habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Rose kwa njia ya simu yake ya mkononi ambapo ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni ndugu yake, akasema;


  • Hii simu imeachwa hapa nyumbani kwani dada (Rose) amepelekwa hospitali Area C, ameng’atwa na nyoka usiku akiwa anaingia getini hapa nyumbani hivyo amepumzishwa hospitali kupewa huduma ya kwanza maana ameng’atwa sana mguu na nyoka alikuwa mkubwa sana.”

Post a Comment

 
Top