0
Muigizaji mkongwe wa filamu nchini, Nuru Nassoro ‘Nora’.
 Baada ya hali ya muigizaji mkongwe wa filamu nchini, Nuru Nassoro ‘Nora’ kubadilika kwa kile kinachodaiwa kuwa ugonjwa unaompanda kichwani, mashehe watano wameletwa kutoka kisiwani Zanzibar ili kuja kufanya maombi maalum ya kumnusuru na hali yake.

Chanzo cha uhakika kilicho karibu na familia ya Nora, kimesema kuwa mashehe hao wanaongozwa na shehe maarufu ndani ya nje ya nchi, Salum Maridhia, ambao tayari wameshawasili jijini Dar es Salaam.

“Unajua Shekhe huyo anafanya sana kazi zake nje ya nchi, lakini kuna ndugu yake alimsaka na kumpata kwa ajili ya kwenda kuondoa maradhi ya Nora, kwa kuwa Shekhe huyo anasifika sana,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.

Gazeti hili liliwasiliana na shehe huyo ili kujua ukweli wa taarifa hizo, ambapo alikiri na kusema anao uwezo wa kuondoa tatizo la muigizaji huyo na hata wengine wa aina hiyo.

“Mimi nilipoambiwa habari hiyo nilikatiza ziara zangu zingine, nimeamua kuja kumuona na baada ya siku saba atakuwa sawa na nitawasaidia na wengine pia” alisema Shehe Maridhawa.

Post a Comment

 
Top