0
VYAMA vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimetoa matokeo ya utafiti uliofanywa sehemu tatu tofauti unaoonyesha mgombea wao wa urais, Edward Lowassa, atapata ushindi wa asilimia 76.

Matokeo ya utafiti huo yalitolewa   Dar es Salaam jana ikiwa ni siku chache tangu   Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Twaweza itoe utafiti wake ambao ulimpa mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli ushindi wa asilimia 65 na Lowassa ushindi wa asilimia 25.

Kabla ya Twaweza,  Chama Cha Mapinduzi (CCM) pia kilitoa utafiti wake uliompa    Dk.   Magufuli ushindi wa asilimia 69.
 
Akitoa ripoti ya utafiti huo jana, Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia alisema Ukawa umefanya utafiti mara tatu ambao ulishirikisha watafiti wa ndani, nje na kwa njia ya mitandao.
 
Mbatia alisema kuwa utafiti wao wa ndani (Ukawa) uliofanywa na wataalam kutoka nje ya nchi unaonyesha kuwa Lowassa atashinda kwa asilimia 74 huku wataalamu wa ndani wakitoa matokeo yanayompa Lowassa ushindi mwingine wa kishindo wa asilimia 76.

“Upo pia utafiti uliofanywa kupitia mitandao ya simu na kuonyesha kuwa Lowassa atashinda kwa asilimia 79,” alisema Mbatia.

Kwa mchanganuo huo, kwa mujibu wa Ukawa, Lowassa atashinda kwa wastani wa asilimia 76.3.

Mbatia alisema wataalam hao walifanya utafiti huo baada ya Lowassa ameshajiunga na umoja huo

Post a Comment

 
Top