0

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, leo  amekihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Sumaye amejiunga rasmi na Ukawa wakati wa mkutano wa wanahabari na viongozi wa Umoja huo,  mkutano uliofanyika mchana wa leo katika ukumbi wa hoteli ya Kunduchi jijini Dar.
Aidha Sumaye hakusema ni chama gani amejiunga nacho, licha ya kubainisha lengo lake kuu la kuondoka CCM ni kwenda kuimarisha Ukawa na kuongeza nguvu kwenye vyama vya upinzani hasa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25.

Post a Comment

 
Top