MABASI ya mwendo wa haraka jijini Dar es Salaam yamezinduliwa rasmi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia, akiambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadick Mecky Said.
Uzinduzi huo wa huduma ya mpito (interim service) umefanyika leo katika kituo cha DART kilichopo nje ya kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo.
Akizungumza na wananchi na wanahabari waliohudhuria hafla hiyo, Hawa Ghasia alisema kuwa jiji la Dar es Salaam ni la pili katika kutekeleza mradi huo baada ya Afrika ya Kusini.Alisema kuwa wananchi wapokee huduma hiyo mpya ya usafiri kutokana hali halisi ya kwenda na wakati tofauti na kuendelea kutumia huduma ambazo haziko kiteknolojia zaidi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadick Mecky Said, akizungumza katika hafla hiyo amesema huduma hiyo itawawezesha wananchi kupunguza idadi ya magari yanayopita barabarani kwa wingi kwa kupanda gari moja tu la DART ambalo litakuwa ni kubwa lenye kutoa usafiri wa haraka.
Aidha amewataka wananchi kuwa makini wakati wanapokuwa barabarani hasa zile ambazo zitakazokuwa zikitumika kwa magari hayo ya mwendo wa haraka, akisema wananchi yeyote atakayepita katikati ya barabara hizo na kusababisha ajari atachukuliwa hatua kali hata kama gari la mwendo wa haraka litamgonga, kwani yeye ndiye atakayeonekana mwenye makosa kama ambavyo treni linapogonga mtu au gari.
“Mwananchi yeyote atakayepita katikati ya barabara hizi na kusababisha ajali atachukuliwa hatua kali mara moja na hata kama gari la mwendo wa haraka litamgonga, yeye ndiye atakayeonekana mwenye makosa huku akifananisha na barabara ya treni.”PICHA NA http://www.globalpublishers.info
Post a Comment