0
Katika kuhakikisha wateja wake kutokuwa nyuma kiteknolojia na kupata huduma bora za mawasiliano ya kisasa kwa kutumia mtandao wa intanet,kampuni ya Vodacom Tanzania imezindua simu mpya ya Smart speed 6 ya gharama nafuu ambayo wananchi wengi wanaweza kumudu kuinunua.
003-phone
Mkuu wa huduma na bidhaa wa Vodacom Tanzania,Samson Mwongela(kushoto)Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo,Jacquiline Materu(katikati)na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu,Wakiwaonyesha simu mpya aina ya Smart speed 6, waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa simu hiyo leo jijini Dar es Salaam yenye kioo kikubwa kinachomuwezesha mtumiaji kusoma na kuangalia taarifa kwa urahisi na yenye kamera ya kisasa na uwezo zaidi wa kuperuzi intaneti ya 4G,Simu hizo zinapatikana kwa bei nafuu kabisa ya shilingi 150,000/- katika maduka na magulio yote ya kampuni hiyo
Akiongea wakati wa uzinduzi wa simu hii Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo,Jacquiline Materu amesema kuwa simu hii imelenga wateja wake wenye vipato vya kawaida ili kuwawezesha kufurahia huduma za kisasa za matumizi ya simu za mkononi za Smartphone ili waweze kwenenda na teknolojia.
“Vodacom siku zote tumekuwa tukiwasikiliza wateja wetu na ndio maana tumeingiza sokoni simu hii ili kuwawezesha kufurahia matumizi ya simu za kisasa za smart ambazo zinawawezesha kupata huduma za internet na program nyinginezo za kurahisisha maisha yao na kuwa murua ikiwemo kupiga picha wazipendazo kwa kutumia simu zao,”Alisema Materu.
Aliongeza kuwa simu hii ya Smart speed 6 ambayo itakuwa inauzwa kwa bei nafuu kabisa ya shilingi 150,000/- ina kioo kikubwa kinachomuwezesha mtumiaji kusoma na kuangalia taarifa kwa urahisi,ina kamera ya kisasa,uwezo zaidi wa kuperuzi intanet ya 4G, nafasi kubwa ya kuweka kumbukumbu na inakaa na betri kwa muda mrefu. Hii ni simu ya kipekee ambayo kila mteja anatakiwa kuwa nayo.
Alisema simu hizi zinapatikana katika maduka na magulio pamoja na matamasha yote yanayofanywa na kampuni yetu nchi nzima.Mteja yeyote atakayenunua simu hii atakuwa na waranti ya mwaka mmoja na pindi iharibikapo atairudisha na kupatiwa ingine mpya.
Aliwataka wateja wa Vodacom na wananchi wengine kwa ujumla kuchangamkia fursa hii na kukamata Smart speed 6 kwa gharama nafuu ili kuendelea kupata taarifa za huduma mbalimbali zinazopatikana kwa kuperuzi mtandao wa intanenti.Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti yetu www.vodacom.co.tz au kurasa zetu za Facebook na Twitter.

Post a Comment

 
Top