0
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea leo November 2 2016, kwa viwanja sita ambako kwa mara ya kwanza timu zote za Dar es Salaam zitakuwa mikoani kupambana kutafuta nafasi bora katika ligi hiyo iliyoanza Agosti 20, 2016 kabla kufifikia ukomo wa mzunguko wa 15, Novemba 12, mwaka huu.
football-2
Vinara ligi hiyo kwenye msimamo msimu wa 2016/17, Simba SC watakuwa wageni wa Stand United kwenye Uwanja wa CCM Kambarage wakati mabingwa watetezi wa taji hilo Young Africans itakaribishwa na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Africans Lyon pia ya Dar es Salaam itakuwa mkoani Pwani kucheza na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani wakati Maafande wengine kutokea mkoani humo – JKT Ruvu watakuwa wageni wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Majimaji ilihali Ndanda itawakabiri Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara huku Toto African ikiwakaribisha Azam kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Ligi hiyo itaendelea Alhamisi Novemba 3, mwaka huu kwa michezo miwili ambayo itafanyika mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa Mwadui kuialika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mwadui Complex huko Shinyanga huku Mbao Fc ikiwa na kibarua kigumu dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Post a Comment

 
Top